Hiki ni kitabu kilichotayarishwa kwa lengo la kuwapatia wasomaji, suluhisho la
matatizo wanayoyapata watu wengi wanapotaka kufahamu ni ipi Dini ya Haki.
Utayarishaji wa kitabu hiki, unatokana na utafiti katika kitabu cha Biblia na Qur'an,
sio tu kwa sababu vitabu hivi viwili ndivyo vitabu mashuhuri vya dini ulimwenguni,
bali kwa sababu ndivyo vimebeba ndani yake ushahidi kuhusu tofauti iliyopo baina ya
maneno ya Mungu na maneno ya Mitume na Manabii. Na ndivyo pia vinavyoweza
kutumika kudhihirisha baadhi ya maneno ya wasomi yaliyoandikwa kisha baadhi ya
watu wakadai kuwa ni maneno ya Mungu, ili wapate kuwapotosha wale ambao
hawajui kusoma vyema.
Mwandishi anatarajia kwamba kitabu hiki kitaweza kutumika kama hatua ya kwanza
ya kutayarisha maisha bora katika jamii zinazozungumza lugha ya Kiswahili. Hayo ni
kwa sababu, hatua ya kwanza katika kuishi maisha bora wakati wote huwa kwanza ni
kumfahamu vyema Mola wa Ulimwengu na kisha kujitahidi kuishi katika njia ya
haki.
Mwanzo wa kuishi katika njia ya haki ni kumwamini Mungu na kuwaamini wote
wale aliyowatuma na kuwatii.
Kwa hivyo, lengo la kitabu hiki ni kumsaidia msomaji kwa risala hii fupi ya
kumuwezesha kupambanua ni ipi dini ya haki.
Hiki ni kitabu kilichotayarishwa kwa lengo la kuwapatia wasomaji, suluhisho la matatizo wanayoyapata watu wengi wanapotaka kufahamu ni ipi Dini ya Haki.
قراءة و تحميل كتاب Al kashaafu Mwangaza Katika Adabu Za Itikafu PDF مجانا
قراءة و تحميل كتاب Masomo katika umuhimu wa Tawhiidi Muhtasari wa kitabu cha Al Usulu AL Thalathah PDF مجانا